Psalms 83

Maombi Kwa Ajili Ya Kushindwa Kwa Adui Wa Israeli

(Zaburi Ya Asafu. Wimbo)


1 aEe Mungu, usinyamaze kimya,
usinyamaze, Ee Mungu, usitulie.

2 bTazama watesi wako wanafanya fujo,
jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao.

3 cKwa hila, wanafanya shauri dhidi ya watu wako,
wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda.

4 dWanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa,
ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.”


5 eKwa nia moja wanapanga mashauri mabaya pamoja,
wanafanya muungano dhidi yako,

6 fmahema ya Edomu na Waishmaeli,
ya Wamoabu na Wahagari,

7 gGebali,
Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti).
Amoni na Amaleki,
Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro.

8 iHata Ashuru wameungana nao
kuwapa nguvu wazao wa Lutu.


9 jUwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani,
na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini
hapo kijito cha Kishoni,

10 kambao waliangamia huko Endori
na wakawa kama takataka juu ya nchi.

11 lWafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu,
watawala wao kama Zeba na Salmuna,

12 mambao walisema, “Na tumiliki nchi
ya malisho ya Mungu.”


13 nEe Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli,
kama makapi yapeperushwayo na upepo.

14 oKama vile moto uteketezavyo msitu
au mwali wa moto unavyounguza milima,

15 pwafuatilie kwa tufani yako
na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.

16 qFunika nyuso zao kwa aibu
ili watu walitafute jina lako, Ee Bwana.


17 rWao na waaibishwe na kufadhaishwa milele,
na waangamie kwa aibu.

18 sHebu wajue kwamba wewe, ambaye jina lako ni Bwana,
kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote.
Copyright information for SwhKC